Vyama vya Sudan Kusini vyaunda jeshi la umoja
2022-04-14 11:51:47| CRI

Vyama  vya Sudan Kusini vimeunda jeshi la umoja ambalo lilikuwa likisubiriwa sana baada ya kuchelewa kwa miezi kadhaa.

Rais Salva Kiir alitoa amri Jumanne kupitia Televisheni ya Taifa (SSBC) na kutangaza wateule kadhaa kuongoza Jeshi la Umoja wa Watu wa Sudan Kusini (SSPDF), magereza, polisi, intelijensia na jeshi la wanyamapori.

Kundi la Harakati za Ukombozi wa Watu wa Sudan la serikali (SPLM/A-IG) chini ya Kiir limechukua asilimia 60 ya muundo wa kamandi na zilizosalia asilimia 40 zimetengwa kwa ajili ya kundi la upinzani la SPLM/A-IO linaloongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar na Muungano wa Upinzani wa Sudan Kusini (SSOA).

Machar na makundi mengine ya upinzani waliwasilisha majina ya maafisa kwa rais Kiir ili kuunganishwa kwenye huduma za usalama.