Timu ya uokoaji ya Afrika Kusini yawatafuta watu wasiojulikana walipo baada ya mvua kubwa kusababisha vifo vya watu 306
2022-04-15 08:57:31| CRI

Mkuu wa Mkoa wa KwaZulu-Natal wa Afrika Kusini Bw. Sihle Zikalala jana alisema mvua kubwa mkoani humo imesababisha vifo vya watu 306, na serikali ya KwaZulu-Natal inaendelea kufanya kazi ya uokoaji.

Rais Cyril Ramaphosa Jumatano alitembelea maeneo yaliyokumbwa na maafa. Serikali imetangaza kuwa mkoa huo umeingia katika hali ya maafa ili kuharakisha kusafirisha vifaa, kujenga upya miundombinu na kufanya kazi ya uokoaji.

Zikalala amesema nyumba, majengo, madaraja, barabara nyingi zimeharibiwa, na upatikanaji wa maji na umeme pia umeathiriwa vibaya, shule zaidi ya 200 zimeharibiwa, na watu 306 wamefariki kutokana na mvua kubwa na mafuriko ya maji.