UNHCR yajenga vifaa vya usafi shuleni ili kuboresha mazingira ya jamii ya wakimbizi nchini Tanzania
2022-04-15 09:03:13| CRI

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi UNHCR linajitahidi kuboresha upatikanaji wa maji, mazingira ya usafi, na huduma za usafi kwa watu binafsi katika jamii inayowahifadhi wakimbizi  kwenye sehemu ya magharibi mwa Kigoma nchini Tanzania.

UNHCR imesema katika taarifa yake kuwa, zana za kutosha za usafi ni haki ya kimsingi ya binadamu, na upatikanaji wake ni muhimu kwa ajili ya kupata maendeleo ya afya, elimu, lishe.

Kutokana na ushirikiano wa mamlaka za mitaa na washirika wake, UNHCR itaendelea kuboresha huduma kwa jamii ya wakimbizi huko Kigoma, wanakoishi wakimbizi wengi kati ya 247,000 nchini Tanzania.

Taarifa hiyo imesema takriban wanafunzi 1,578 wa shule ya msingi wamenufaika na ujenzi wa vyoo viwili.