Wanaanga waliokwenda anga za juu na Chombo cha Shenzhou No.13 warudi salama duniani
2022-04-16 11:57:08| CRI

Chombo cha Shenzhou No. 13 cha China kilichobeba wanaanga watatu kimetua salama katika eneo la kutua la Dongfeng katika mkoa wa Mongolia ya Ndani. Wanaanga hao Bw. Zhai Zhigang, Bi. Wang Yaping na Bw. Ye Guangfu wametoka katika chombo hicho na wana hali nzuri ya kiafya.

Wanaanga hao wamekaa kwenye kituo cha anga za juu cha China kwa zaidi ya siku 180, muda ambao ni mrefu zaidi kwa safari moja katika historia ya safari za anga za juu ya China.