Sudan yadai tena umiliki wa eneo la Fashaga
2022-04-18 09:01:34| CRI

Sudan imethibitisha tena umiliki wake kwa eneo la mpakani la Fashaga linalogombewa kati yake na Ethiopia.

Kaimu waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Ali Al-Sadiq, ametoa taarifa akisisitiza kuwa Fashaga ni ardhi ya Sudan alipokutana na mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Pembe ya Afrika Bi. Hanna Tetteh. Waziri huyo amesema mazungumzo ni njia bora ya kutatua mgogoro huo kati ya nchi hizo mbili.

Tangu mwezi Septemba mwaka 2020, mvutano na mapigano katika eneo hilo la mpakani kati ya Sudan na Ethiopia vimezidi kuongezeka, na mwezi Desemba mwaka huo, jeshi la Sudan lilidai kuwa limedhibiti eneo hilo.