Kampuni za China nchini Misri zatoa mchango kwa watu wenye mahitaji katika mwezi wa Ramadhani
2022-04-18 08:35:33| CRI

Kampuni zaidi ya 30 za China nchini Misri zimeshiriki kwenye shughuli ya hisani ya mwezi wa Ramadhani inayolenga kuchangia pauni milioni moja za Misri kwa familia zenye mahitaji.

Shughuli hiyo ya mwaka huu ni ya awamu ya nane tangu ilipoanzishwa na Baraza la Wafanyabiashara wa China nchini Misri mwaka 2015.

Akiongea kwenye shughuli hiyo iliyofanyika Jumamosi, Balozi wa China nchini Misri Liao Liqiang, amesema watu wa China wana maadili ya jadi ya kutoa na kulipa fadhila, na kampuni za China kutoa msaada kwenye shughuli hiyo, kunaakisi urafiki mkubwa kati ya watu wa nchi hizo mbili.