Watu sita waliwa na mamba katika mto Ruvu nchini Tanzania
2022-04-18 09:05:56| CRI

Mwenyekiti wa kijiji cha Kimaramisale kilichopo katika wilaya ya Dutumi mkoani Pwani nchini Tanzania Bw. Salum Bong’o, amesema kuwa takriban watu sita wameliwa na mamba katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2022 katika Mto Ruvu.  

Bw. Salum Bong’o amesema hayo akiongea na mbunge wa wilaya ya Kibaha kijiji Bw. Michael Mwakamo. Amesema kuwa baba yake ni mmoja wa wahanga, watu hao sita walishambuliwa na kuliwa na mamba wakati wakichota maji kwenye mto huo. Wanakijiji wameitaka idara ya wanyamapori katika wizara ya maliasili na utalii kuwakamata mamba hao.