Tume ya Umoja wa Afrika yapongeza kikosi cha Uganda kwa kupambana na magaidi ya al-Shabab nchini Somalia
2022-04-18 09:21:55| CRI

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia ATMIS imekipongeza kikosi cha Uganda kinachomaliza muda wake kwa kuimarisha mapambano dhidi ya magaidi wa kundi la al-Shabab katika eneo la pwani ya Barawe, kusini mwa Somalia.

Kamanda wa kikosi cha ATMIS Bw. Diomede Ndegeya amewatunuku nishani na vyeti askari wa kikundi cha 32 kwa mchango wao katika mchakato wa ujenzi wa amani unaoendelea nchini Somalia.

Bw. Ndegeya amesema baada ya kupelekwa katika vituo tofauti vya kijeshi huko Barawe na Beldamin, askari hao walifanya kazi na kudumisha operesheni kuu za kijeshi za kupunguza nguvu ya kijeshi ya kundi la al-Shabab.