Kenya yaanzisha ukaguzi wa kawaida forodhani kwa mizigo inayoagizwa kutoka nje
2022-04-20 09:03:42| CRI

Mkurugenzi wa Shirika la viwango la Kenya (KEBS) Bw. Bernard Njiraini amesema Kenya imeanza ukaguzi wa mizigo yote inayoagizwa kutoka nje.

Akiongea mjini Nairobi Bw. Njiraini amesema hatua hiyo iliyokuwa inafanyika kwenye nchi zinakotoka bidhaa hizo sasa imefika mwisho, na badala yake cheti kinachotolewa na Kenya ndio kitatolewa kwa bidhaa zinazokidhi vigezo vya ndani. Amesisitiza kuwa bidhaa ambazo hazitaonekana kukidhi vigezo zitarudishwa zilikotoka au zitateketezwa kwa gharama za mwagizaji.

Bw. Njiraini pia amesema wameanzisha utaratibu wa njia nne za ukaguzi, ili kuhakikisha hakuna usumbufu kwenye uagizaji wa bidhaa na kuhakikisha kuwa hakuna bidhaa za viwango vya chini zinaingia nchini Kenya.