China na Ghana zaahidi kuimarisha ushirikiano
2022-04-20 09:27:30| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na mwenzake wa Ghana Bi Shirley Ayorkor Botchwey, wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na kutoa mwito kujenga uhusiano wa karibu zaidi.

Bw. Wang amesema China inatilia maanani urafiki wa jadi kati yake na Ghana, huku akieleza kuwa uhusiano kati ya pande hizo mbili umeimarishwa na kuendelezwa chini ya uongozi wa marais wa nchi mbili.

Amesema hasa tangu mlipuko wa COVID-19, China na Ghana zimeungana mkono kukabiliana na matatizo, na urafiki kati ya pande mbili umezidi kuimarishwa.

Pia ameishukuru Ghana kwa kushikilia sera ya kuwepo kwa China moja, na kusema China inaamini kuwa pande mbili zitaendelea kuzidisha uaminifu wa kisiasa na kulinda kwa pamoja ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Bi Botchwey amesema kuwa Ghana inathamini urafiki kati yake na China na itafuata kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja.