Kenya yazindua app ya simu ya lugha ya ishara ili kuhimiza ushirikishi wa kijamii na kiuchumi
2022-04-21 08:58:34| CRI

Kenya imezindua app ya simu ya kutoa huduma za kutafsiri lugha ya ishara moja kwa moja ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhimiza ushirikishi wa kijamii na kiuchumi.

Katibu mkuu katika Wizara ya Habari, Mawasiliano na TEHAMA, Uvumbuzi na Masuala ya Vijana, Bibi Maureen Mbaka amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa app hiyo ya simu iitwayo “assitALL” itaziba pengo la mawasiliano kati ya watu wenye ulemavu wa kusikia na pande za tatu kwenye mambo ya afya, elimu ya juu, mfumo wa sheria, huduma za serikali na fedha.

Takwimu zinaonesha kuwa sasa kuna watu zaidi ya laki 2.6 wenye ulemavu wa kusikia nchini Kenya.