Tanzania yaanza utafiti wa kijiolojia kuhusu madini yake
2022-04-21 08:59:12| CRI

Serikali ya Tanzania inafanya uchunguzi wa kijiolojia unaolenga kutambua na kusasisha data na rekodi za madini yake.

Naibu waziri wa madini Bw. Steven Kiruswa amesema taarifa zitakazokusanywa kwenye utafiti huo ambao utatekelezwa na Idara ya Uchunguzi wa Kijiolojia ya Tanzania, zitatangazwa kwa umma.

Bw. Kiruswa ameliambia bunge mjini Dodoma kuwa uchunguzi huo unalenga kuhakikisha Watanzania wote wanapewa taarifa ipasavyo kuhusu hazina ya madini iliyopo kwenye maeneo wanakoishi.