Lugha ya kichina inaleta mafungamano ya kiutamaduni miongoni mwa vijana wa Namibia
2022-04-21 09:15:17| CRI

Wakati siku ya kimataifa ya lugha ya Kichina imeadhimishwa jana kote duniani, imefahamika kuwa utamaduni wa China unaendelea kuwa na mvuto kwa vijana wa Namibia wakati vijana hao wakiendelea kujifunza zaidi lugha ya kichina.

Vijana wa vyuo vikuu wanaoendelea na masomo yao katika taasisi ya Confucius mjini Windhoek wanaona kuwa, mbali na lugha ya kichina kuongeza idadi ya lugha wanazoweza kuongea, pia lugha hiyo inaondoa kikwazo cha mawasiliano.

Mmoja wa wanafunzi wa lugha hiyo amesema lugha ya kichina ni lugha inayoongewa na watu wengi zaidi duniani, na popote unapokuwa duniani kwa namna moja au nyingine utakutana na lugha ya kichina.

Wanafunzi wengine wamewataka watu kuondoa imani kuwa lugha ya kichina ni ngumu.