Vikosi vya Somalia vyawaua wapiganaji 10 wa kundi la Al-Shabaab kwenye mkoa wa kati
2022-04-22 08:48:41| CRI

Vikosi maalum vya Somalia vimewaua wapiganaji zaidi ya 10 wa kundi la Al-shabaab na kuwajeruhi wengine kwenye operesheni ya usalama iliyofanyika katikati ya nchi hiyo.

Maofisa wa jeshi la Somalia wameiambia Radio ya Taifa ya Somalia kuwa vikosi maalum vimefanya operesheni dhidi ya kundi hilo kwenye vijiji kadhaa katika eneo la Mudug, kwenye vijiji vya Qararow, Kalaxiran, Goryale, Dhumale, Caad, Gabdhale na Waable.

Jeshi la Somalia limeimarisha operesheni za usalama dhidi ya kundi la Al-shabaab ili kuyakomboa maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa kundi hilo.