Kagame ajibu kuhusu makubaliano ya kutoa hifadhi kwa wakimbizi yaliyofikiwa kati ya Rwanda na Uingereza
2022-04-22 09:12:34| CRI


Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema makubaliano ya kutoa tena hifadhi kwa wakimbizi yaliyofikiwa na Rwanda na Uingereza yanalenga kutatua msukosuko wa wakimbizi duniani, na utoaji tena wa hifadhi si usafirishaji haramu wa binadamu. Amesema watu wanatakiwa kufahamu kwa kina historia, na kufahamu msingi wa uhusiano wa kiwenzi kati ya nchi hizo mbili kwenye masuala ya wahamiaji. Pia ametaja amri iliyotolewa na serikali mwaka 2018 kuhusu kuwapokea wakimbizi wa Libya.

Imefahamika kwamba serikali ya Rwanda, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika mwezi Septemba mwaka 2019 walisaini makubaliano ya kuanzisha mfumo wa mpito wa kuhamisha wakimbizi kutoka Libya.

Lakini makubaliano hayo yameleta migongano. Aprili 18 Eritrea ilitoa taarifa ikisema, makubaliano yaliyofikiwa kati ya Rwanda na Uingereza ni ya aibu. Taarifa imesema baadhi ya nchi zinatekeleza sera ya kimkakati ya kupunguza idadi ya watu katika nchi nyingine, kutokana na sababu fulani za kisiasa zisizoweza kutajwa.