Kenya kuandaa mbio za marathon kwenye barabara ya mwendokasi ya Nairobi iliyojengwa na kampuni ya China
2022-04-22 08:47:52| CRI

Waandaaji wa mbio za marathon wa Kenya wamesema wanariadha maarufu wa Kenya na raia wa kawaida watapata fursa ya kukimbia kwenye barabara ya mwendokasi ya Nairobi iliyojengwa na kampuni ya China, kwenye mbio zilizopangwa kufanyika tarehe 28 Mei, kabla ya kufunguliwa rasmi kwa barabara hiyo yenye kilometa 27.

Taarifa iliyotolewa na waandaaji wa mbio hizo ambao ni wizara ya michezo ya Kenya na Mfuko wa maendeleo ya jamii, imesema mji wa Nairobi unawaalika wakimbiaji wote kwenye ufunguzi wa makala ya kwanza ya mbio hizo, ambazo zitakuwa na mbio za kilometa 42, kilometa 21, kilometa 10 na kilometa 5.

Kwa mujibu wa mamlaka ya barabara kuu ya Kenya, mkandarasi wa China sasa yuko kwenye hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kabla ya kuzinduliwa na Rais Uhuru Kenyatta.