Jeshi la Nigeria latuma askari 173 nchini Guinea-Bissau kutekeleza jukumu la kulinda utulivu
2022-04-22 09:55:54| CRI

Kamanda mkuu wa jeshi la Nigeria Jenerali Oluwafemi ametangaza kuwa, jeshi la Nigeria litatuma askari 173 nchini Guinea-Bissau ili kuimarisha usalama, na kutekeleza jukumu la kulinda utulivu katika eneo la jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).

Tarehe 1 Februari jaribio la mapinduzi lilitokea nchini Guinea-Bissau, ambapo rais Umaro Sissoco Embalo na waziri wa baraza la mawaziri wa nchi hiyo walishambuliwa na watu wenye silaha. Jeshi la Guinea -Bissau lilizuia jaribio hilo. Tarehe 3 ECOWAS ilitangaza kutuma kikosi cha kulinda utulivu nchini Guinea Bissau ili kuisaidia nchi hiyo kulinda usalama.