Wanajeshi sita wauawa katika mashambulizi katikati ya Mali
2022-04-25 08:31:10| cri


 

Jeshi la Mali jana limethibitisha kuwa, wanajeshi sita waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyotokea karibu wakati mmoja katikati ya nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya habari na uhusiano wa umma ya Jeshi la Mali (Dirpa) imesema, magaidi 11 pia waliuawa katika mashambulizi yaliyotokea mapema Jumapili huko Niono, Bapho, na kambi ya Sevare.