Watu 15 wauawa katika mapigano ya kikabila nchini Sudan
2022-04-25 08:38:31| CRI

 

Mapigano ya kikabila katika eneo ya Kirainik, mkoa wa Darfur Magharibi yameanza tena jana jumapili.

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu vifo na majeruhi, lakini vyanzo vya habari vinadai kuwa, watu 15 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mapigano hayo, huku nyumba kadhaa zikichomwa moto katika mapigano yaliyoanza ijumaa iliyopita.

Kaimu katibu mkuu wa serikali ya mkoa wa Darfur Magharibi Mohamed Zakaria amesema, eneo la Kirainik lilishambuliwa kwa pande zote, na hali ndani ya eneo hilo ni mbaya.

Wakati huohuo, Gavana wa eneo la Darfur Minni Arko Minnawi amesisitiza kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa, kuna haja ya vikosi vya usalama vya kawaida kutekeleza majukumu yao katika kudumisha usalama na utulivu mkoani humo.