Viongozi wa Rwanda na Uganda wakubaliana kukabiliana na ukosefu wa usalama mashariki mwa DRC
2022-04-25 08:39:28| CRI

Rais wa Uganda Yoweri Museveni na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame aliye ziarani nchini Uganda, wamekubaliana kuendeleza juhudi za pamoja kwa ajili ya usalama na utulivu wa kikanda ili kukabiliana na ukosefu wa usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Akizungumza katika mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mjini Nairobi, Kenya, na kuongozwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Rais Museveni amesema matatizo yanayoathiri kanda hiyo kama mgogoro nchini DRC yanahitaji juhudi za pamoja kutoka kwa nchi wanachama wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake, rais Kagame amesema vongozi na pande zote husika wanapaswa kuzungumza ili kutatua kikamilifu mgogoro wa nchini DRC.

Mkutano huo umeyataka makundi yote yenye silaha nchini DRC kushiriki bila masharti katika mchakato wa kisiasa ili kutatua malalamiko yao.