Tanzania kutokomeza Malaria ifikapo mwaka 2030
2022-04-26 09:13:57| CRI

Tanzania imeadhimisha Siku ya Malaria Duniani ikiahidi kutokomeza ugonjwa huo hatari nchini humo ifikapo mwaka 2030.

Waziri wa Afya wa nchi hiyo Ummy Mwalimu amesema serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inatekeleza mpango mkakati wa miaka mitano kuanzia mwaka 2021 hadi 2025, unaolenga kupunguza maambukizi ya malaria kutoka asilimia 7.5 ya mwaka 2017 hadi asilimia 3.5 ya mwaka 2025.

Ummy amesema mpango huo ni pamoja na kutokomeza mbu wanaoeneza malaria, kuimarisha utafiti na matibabu ya malaria na kuweka mazingira safi.