Mgonjwa wa pili wa Ebola afariki dunia DRC
2022-04-27 08:37:43| cri


Shirika la Afya Duniani (WHO) jana limethibitisha kuwa, baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutangaza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mwisho wa wiki iliyopita, kesi ya pili ya Ebola imeripotiwa kwenye Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Kupitia mtandao wa Twitter, Shirika hilo limesema, jumatatu wiki hii, mamlaka za afya nchini DRC zilithibitisha mgonjwa wa pili wa Ebola, mwanamke mwenye umri wa miaka 25 amefariki dunia. Mwanamke huyo alianza kuonyesha dalili za ugonjwa huo siku 12 zilizopita.

DRC inashuhudia mlipuko wa 14 wa Ebola tangu mwaka 1976, huku mlipuko wa sasa ukiwa ni 6 tangu mwaka 2018.