Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Sudan, Bw. Mohamed El Hacen Ould Lebatt alisema, mazungumzo ya kina kati ya makundi ya kisiasa ya Sudan yamepangwa kufanyika kuanzia Mei 10 hadi Mei 12.
Sudan imekumbwa na mzozo wa kisiasa baada ya kamanda mkuu wa Jeshi la Sudan Bw. Abdel Fattah Al-Burhan kutangaza hali ya hatari Oktoba 25, 2021 na kuvunja Baraza la Mpito na serikali.
Kuanzia wakati huo, maandamano makubwa yamefanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum na miji mingine, yakidai kurejeshwa kwa utawala wa kiraia.