Makubaliano ya kusimamisha mapigano nchini Sudan Kusini huenda yakavunjika
2022-04-29 10:00:35| cri


Mwneyekiti wa Utaratibu wa Mpito wa Kusimamisha Vita (CTSAMVM) nchini Sudan Kusini Asrat Denero Amad ameonya kuwa, makubaliano ya kusimamisha mapigano nchini humo yanakabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na vurugu zinazoendelea katika eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Unity na Upper Nile.

Bw. Amad ameonya kuwa, makubaliano hayo yako hatarini kutokana na mapigano kati ya makundi yaliyotengana ya chama kikuu cha upinzani nchini Sudan Kusini cha SPLM-IO.

Makubaliano ya kusimamisha vita yaliyosainiwa Desemba, 2017 kati ya chama hicho kinachoongozwa na Makamu wa Kwanza wa rais Riek Machar na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir yamedumu, licha ya mapigano katika baadhi ya maeneo yaliyo ndani zaidi nchini humo.