China na Afrika zinapaswa kutafuta njia za kidemokrasia zinazoendana na hali ya nchi husika
2022-04-29 09:59:59| cri


Wawakilishi wa nchi za Afrika zinazotumia lugha ya Kifaransa walioshiriki semina ya siku mbili iluyoandaliwa na China kuhusu “Utafiti na Utekelezaji wa Demokrasia katika Sheria za China na Afrika” wamesema, China na Afrika zinapaswa kwa pamoja kutafiti njia za demokraisa zinaendana na mazingira ya kitaifa ili kutoa mchango katika kuboresha maisha ya watu na kuimarisha demokrasia ya uhusiano wa kimataifa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Senegal inayoshughulika masuala ya kimataifa, raia wa Senegal walioko nje ya nchi na maingiliano ya Afrika, Pape Biram Toure amesema, semina hiyo imetoa jukwaa kwa wabunge wa China na Afrika kuimarisha zaidi ushirikiano wao ambao tayari ni imara.

Naye mjumbe wa Kamati ya Bunge la Gabon inayoshughulikia ushirikiano kati ya China na Gabon Boris Wada amesema, mchakato mzima wa mfumo wa demokrasia ya watu wa China unaendana na mazingira ya nchi hiyo, na mfumo huo unawakilisha sauti ya Wachina, na hivyo kutoa mfano mzuri kwa nchi nyingine kujifunza kupitia mfumo huo.