Vikosi vya mseto vyawaua wapiganaji 22 wa Boko Haram katika eneo la Ziwa Chad
2022-05-02 10:14:54| CRI

Takriban wapiganaji 22 wa kundi lenye itikadi kali la Boko Haram waliuawa wakati wa operesheni ya hivi majuzi kwenye ukingo wa Ziwa Chad na wanajeshi wa Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Pamoja (MNJTF).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa MNJTF Kamarudeen Adegoke siku ya Jumapili na kuipta shirika la habari la China Xinhua, wanajeshi wa kikosi kazi hicho cha pamoja cha kikanda walitekeleza operesheni ya kuondoa baadhi ya ngome za Boko Haram karibu na Tumbun Rago, mji ulioko katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria pembezoni mwa Ziwa Chad.

Adegoke alisema licha ya jibu kali la magaidi wa Boko Haram, askari wa ardhini walipitia vikwazo kadhaa na kusafisha njia zilizochimbwa, jambo ambalo liliwafanya kukabiliana na waasi hawa.

Tathmini ya uharibifu wa vita inaonesha kuwa wapiganaji 20 waliuawa katika operesheni hiyo na wawili waliokimbia pia waliuawa na wanajeshi katika doria ya kuwafuatilia katika eneo hilo.

MNJTF ni vikosi vya mseto vilivyoundwa na nchi zikiwemo Cameroon, Chad, Niger, Nigeria na Benin ili kupambana na Boko Haram tawi la IS Jimbo la Afrika Magharibi ISWAP, ambalo linatishia utulivu wa eneo la Ziwa Chad.