ATMIS yaikabidhi Somalia silaha zilizonaswa wakati wa mashambulizi dhidi ya al-Shabab
2022-05-02 10:13:27| CRI

Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema imeikabidhi serikali ya Somalia silaha zilizokamatwa wakati wa operesheni za usalama dhidi ya kundi la al-Shabab, kama sehemu ya juhudi za kuwapunguza kasi wanamgambo hao.

Naibu mkuu wa ATMIS Bi. Fiona Lortan amesema kwenye taarifa kwamba serikali ya Somalia na ATMIS zitaandika na kusajili silaha na vifaa vyote vya kijeshi vilivyokamatwa wakati wa mashambulizi au wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Kamanda wa kikosi cha Uganda cha tume ya ATMIS Bw. Keith Katungi amesema urejeshaji wa silaha kutoka kwa al-Shabab unalenga kudhibiti matumizi yao makubwa.

Kamanda wa vikosi vya ardhini wa SNA Bw. Mohamed Tahlil Bihi amesifu ushirikiano kati ya ATMIS na SNA katika juhudi za kurejesha amani na utulivu, kabla ya kuhamisha majukumu ya usalama kwa vikosi vya usalama vya Somalia.