Kenya yachukua hatua kuzuia maambukizi ya Ebola ya kuvuka mipaka ya nchi
2022-05-02 10:16:58| CRI

Mamlaka ya Afya ya Kenya imesema, baada ya mgonjwa wa Ebola kuripotiwa tena nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hivi sasa Kenya iko katika kiwango cha juu cha tahadhari.

Mkurugenzi wa Kituo cha utafiti wa virusi katika Taasisi ya Matibabu ya Kenya amesema, vituo vyote vya kuingia nchini humo vimejiandaa kufanya upimaji wa virusi vya Ebola, huku Idara za Afya zikifuatilia kwa makini shughuli za kuvuka mipaka ya nchi, haswa kutoka Jamhuri ya Kidmokrasia ya Kongo. Ikiwa mgonjwa wa Ebola atatambuliwa, watu wanaohusika watatengwa, na idara husika zitafanya upimaji zaidi.

Shirika la Afya Duniani WHO kanda ya Afrika Aprili 23 lilitoa taarifa ikisema, mgonjwa mmoja wa Ebola amethibitishwa nchini humo. Hii ni kesi mpya ya Ebola baada ya nchi hiyo kutangaza kumalizika kwa maambukizi ya Ebola mwezi Disemba mwaka 2021. WHO imetangaza kuwa itapeleka timu tatu za utoaji wa chanjo kwenye maeneo yaliyo hatarini zaidi, ili kuzuia maambukizi mapya ya virusi.