Maonyesho ya biashara ya utalii barani Afrika yanaanza mjini Durban
2022-05-03 09:44:11| CRI

Maonyesha ya biashara ya utalii barani Afrika (Africa's Travel Indaba) yameanza mjini Durban, nchini Afrika Kusini.

Naibu Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini Bw. Fish Mahlalela amesema kuwa licha ya vikwazo vya COVID-19, utalii umeonyesha uthabiti na kuimarika.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Utalii wa Afrika Kusini Bw. Themba Khumalo amesema maonesho hayo yamejaa fursa zinazoleta matokeo muhimu kwa wajumbe wote, kutoka mazungumzo ya biashara yanayozingatia mada zinazohusiana na utalii, hadi soko la kasi linalolenga kuonesha mpangilio wa biashara ndogo za Afrika Kusini nzima. Mbali na hapo maonesho hayo pia yanatoa fursa nyingi za mawasiliano.

Maonyesho ya biashara ni moja ya matukio makubwa zaidi ya soko la utalii kwenye kalenda ya Afrika na moja ya matukio matatu bora ya aina yake ambayo ni lazima kutembelea kwenye kalenda ya kimataifa.