Rais wa Burundi atoa tuzo kwa wafanyakazi bora akiwemo mfanyakazi wa China wakati wa Siku ya Wafanyakazi Duniani
2022-05-03 09:48:04| CRI

Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi Jumatatu alitoa tuzo kwa wafanyakazi na mashirika bora akiwemo raia wa China, wakati nchi hiyo ilipoadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani.   

Siku hiyo iliadhimishwa katika Uwanja wa Michezo wa Umuco huko Muyinga, mkoa wa Muyinga ulioko kaskazini mashariki mwa Burundi.

Mashirika na watu wengi waliopewa tuzo wapo katika sekta ya kilimo.

Rais Ndayishimiye amesema mtaalamu wa China wa kilimo cha mpunga vilevile ni mmoja kati ya watu wanaochangia sana maendeleo ya Burundi. Alimsifu Yang Huade, ambaye amesema tani 10 za mpunga zinaweza kuvunwa katika shamba la hekta moja tu, akiongeza kuwa Yang ametoa mchango mkubwa katika Kituo cha utafiti wa mpunga cha Gihanga mkoani Bubanza.

Vilevile Rais Ndayishimie ameeleza kuwa Yang anajulikana katika maeneo mengine kama vile Karusi na Gitega ambapo mpunga hulimwa, ili kuwasaidia wakulima kwa ujuzi na ufundi wake.