UM wasititiza jukumu la vyombo vya habari vya Somalia katika maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya Habari Duniani
2022-05-04 10:48:37| CRI

Mjumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Bw. James Swan amesisitiza jukumu muhimu la vyombo vya habari vya nchi hiyo kwa jamii ya Somalia na haja ya kuhakikisha uwezo wao wa kufanya kazi kwa usalama na uhuru.

Bw. Swan amesema hayo katika taarifa yake iliyotolewa mjini Mogadishu, wakati wa madhimisho ya Siku ya Vyombo vya Habari Duniani.

Ameongeza kuwa waandishi wa habari nchini Somalia bado wanakabiliwa na tishio la kimwili katika maeneo mengi na wanapaswa kuwa na uwezo wa kufanya kazi zao kwa uhuru bila woga au vitisho, kwani vyombo vya habari vya Somalia ni sehemu muhimu ya ukuaji wa demokrasia.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mwandishi mmoja wa habari ameuawa na wengine wawili kujeruhiwa kuanzia mwezi Mei mwaka jana, na waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari 64 wamekamatwa wakati wakifanya kazi zao katika kipindi hicho.