Uzalishaji wa mahindi nchini Zimbabwe wapungua kwa asilimia 43 kutokana na uhaba wa mvua
2022-05-05 10:37:39| CRI

Waziri wa Habari wa Zimbabwe Bi. Monica Mutsvangwa amesema kuwa pato la mahindi la Zimbabwe linatarajiwa kupungua kwa asilimia 43 katika msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022 kutokana na uhaba wa mvua.

Akitoa taarifa kwa wanahabari baada ya baraza la mawaziri, Bi. Mutsvangwa amebainisha kuwa tumbaku, mojawapo ya zao linazoingiza fedha nyingi za kigeni nchini Zimbabwe, inatarajiwa kupungua kwa asilimia 8 ambayo ni hadi tani 183,725 kutoka tani 200,245 za msimu uliopita.

Makadirio hayo ni kwa mujibu wa matokeo ya ripoti ya tathmini ya mazao na mifugo ya duru ya pili ambayo iliwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri na Waziri wa Kilimo Anxious Masuka. Uzalishaji wa mazao mengine kama vile soya, mpunga, viazi mbatata na viazi vitamu unatarajiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa mwaka huu.