Somalia yaamua tarehe ya kufanya uchaguzi wa rais
2022-05-06 10:20:24| CRI

Bunge la Somalia lilitangaza jana Alhamisi kuwa uchaguzi wa rais uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu utafanyika Mei 15 huko Mogadishu, mji mkuu wa nchi hiyo.

Kamati ya pamoja ya bunge inayoandaa uchaguzi wa rais imesema wabunge 329 kutoka mabunge yote mawili – 54 kutoka seneti au baraza la juu la bunge na 275 kutoka baraza la chini la bunge – watamchagua rais wa awamu ya kumi wa nchi hiyo. 

Kamati hiyo ilisema wagombea urais watalihutubia bunge Mei 11 na 12 kuhusu sera zao kabla ya upigaji kura.

Uchaguzi wa rais utafanyika sambamba na siku ya kihistoria kwani nchi hiyo pia itaadhimisha miaka 79 ya Shirikisho la Vijana la Somalia lililoanzishwa Mei 15, 1943, na wanaharakati vijana 13 ambao waliongoza mapambano kwa ajili ya umoja na uhuru wa Somalia katika miaka ya 40 na 50 katika karne 20.