Watu zaidi ya elfu 16 wauawa kwenye vurugu za watu wenye itikadi kali huko Afrika Magharibi
2022-05-06 10:16:48| CRI

Waziri wa ulinzi wa Ghana Bw. Dominic Nitiwul jana alipohudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Kamati ya wanadhimu wakuu wa ulinzi katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) amesema, katika miaka mitatu iliyopita watu wasiopungua 16,726 waliuawa kwenye vurugu za watu wenye itikadi kali huko Afrika Magharibi.

Nitiwul amesema kumekuwa na mashambulizi 5,306 yanayohusiana na ugaidi ambayo yalitokea kwenye eneo hilo, hali ambayo ilisababisha vifo vya watu 16,726, na wengine maelfu kujeruhiwa, huku mamilioni ya watu wakipoteza makazi yao.

Ameongeza kuwa inapaswa kuchukuliwa hatua madhubuti ili kupata uungaji mkono kwa ajili ya nchi ambazo sasa zinapambana na hali isiyo salama baharini, janga la ugaidi na vurugu za watu wenye itikadi kali.