Ethiopia yatangaza kupandisha bei ya mafuta kwa asilimia 16
2022-05-09 08:35:23| CRI

Wizara ya Biashara na Ushirikiano wa Kikanda (MoTRI) ya Ethiopia imetangaza uamuzi wa kupandisha bei ya mafuta kwa asilimia 16 kuanzia Jana jumapili.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na wizara hiyo, uamuzi wa kupandisha bei ya petroli umesababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta duniani. Katika miezi minne iliyopita Ethiopia haikupandisha bei ya bidhaa za petroli, hatua ambayo imesababisha nakisi ya kila mwezi ya Birr bilioni 10 na kuleta shinikizo kubwa la kifedha kwa serikali.

Wizara hiyo pia imetoa onyo kwenye tangazo hilo kwamba itachukua hatua za kisheria na kiusimamizi dhidi ya "mashirika haramu" yanaokusudia kutumia fursa hiyo kuleta uhaba wa makusudi au kuongeza bei kwa bidhaa za msingi.