UM yatoa dola milioni 19 za kimarekani kuisaidia Sudan Kusini kukabiliana na mafuriko
2022-05-09 08:49:37| CRI

Shirika la uratibu wa misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa UNOCHA, limesema limetoa dola milioni 19 za kimarekani kuisaidia Sudan Kusini kujiandaa kukabiliana na mafuriko yanayotarajiwa kutokea wakati wa msimu wa mvua.

Shirika hilo limesema fedha hizo zitatumiwa kusaidia mashirika kujiandaa kuwalinda watu katika kambi ya Bentiu ya watu waliopoteza makazi, na sehemu zilizoko karibu katika jimbo la Unity, ambako ni moja ya sehemu zenye hatari ya kuathiriwa vibaya zaidi na mafuriko.

Mratibu wa mambo ya kibindamu nchini Sudan Kusini Sara Beysolow Nyanti ametoa taarifa ikisema katika miaka mitatu iliyopita, mafuriko makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa yaliharibu maisha ya watu. Fedha hizo zitawezesha mashirika ya kibinadamu kupunguza athari zitakazoletwa na misukosuko mingine kupitia kujiandaa na kuilinda mapema jamii katika eneo la Bentiu.