Wakenya wapata ushindi kwenye ufunguzi wa mbio za Nairobi City Marathon
2022-05-09 08:20:48| CRI

Wanariadha wa Kenya Brimin Mison na Agnes Barsosio wamekuwa washindi wa mbio za Marathon za Nairobi zilizofanyika jana na kujishindia dola elfu 60 kila mmoja.

Mbio hizo zilizofanyika kwenye barabara mpya ya Nairobi Experessway iliyojengwa na kampuni ya China, zimeshirikisha wanariadha elfu 10, na kutajwa kuwa mbio zenye tuzo kubwa ya fedha barani Afrika.

Mbio hizo zimeandaliwa na wizara ya michezo, utamaduni na urithi wa kale ya Kenya na kufunguliwa na Rais Uhuru Kenyatta.