Watoto milioni 4.5 nchini Zambia wapata chanjo dhidi ya polio
2022-05-10 09:22:30| CRI

Waziri wa afya wa Zambia Bibi Sylvia Masebo amesema watoto wapatao milioni 4.5 wenye umri chini ya miaka mitano, wamepata chanjo dhidi ya polio kutokana na kampeni ya chanjo ya matone iliyozinduliwa mwezi Machi mwaka huu.

Bibi Sylvia amesema wizara hiyo imefurahishwa na uungaji mkono wa wazazi kwa mpango huo, uliozinduliwa kama hatua ya kuzuia mlipuko wa polio uliotokea katika nchi jirani ya Malawi. Amesema programu hiyo imezinduliwa katika majimbo matatu ya nchi hiyo yaliyo katika hatari kubwa, na baadaye ilienezwa katika majimbo yote yanayojumuisha wilaya zote 116.