Mashirika makubwa ya uchimbaji wa madini ya Afrika yatoa mwito wa kuanzishwa mnyororo wa thamani
2022-05-10 09:19:09| CRI

Mashirika makubwa ya uchimbaji wa madini barani Afrika yamesema kuna fursa kubwa na matarajio mazuri kwenye sekta ya madini barani Afrika kwenye “metali za kijani’ na madini ya aina nyingine, huku yakitarajia uwekezaji wenye sekta hiyo utaleta manufaa zaidi kwa jamii za wenyewe kupitia kuanzisha mnyororo wa thamani.

Akiongea kwenye mkutano wa kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya madini Afrika kusini, Indaba, waziri wa madini na nishati wa Afrika Kusini Bw. Gwede Mantashe amesema Afrika ina madini mengi ambayo hayajachimbwa kama vile Lithium, shaba, cobalt, nickel na zink, na mpito kuelekea siku za baadaye zenye uchafuzi mdogo wa hewa ya ukaa, utahimiza mahitaji ya madini kama hayo.

Rais Hakainde Hichilema wa Zambia amesema sekta ya madini inaweza kuwa mchangiaji mkubwa wa uchumi, na nchi hiyo inakaribisha ushirikiano na wadau wa sekta ya madini.