EABC lashuhudia mahusiano ya kibiashara kuongezeka baada ya DRC kujiunga na Jumuiya ya EAC
2022-05-11 08:46:50| CRI

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki EABC limesema mahusiano ya biashara katika kanda ya Afrika Mashariki yanatarajiwa kuongezeka kufuatia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC.

Taarifa iliyotolewa na baraza hilo inasema mwaka jana thamani ya bidhaa zilizonunuliwa na nchi za jumuiya hiyo kutoka DRC ilifikia dola milioni 49.2 za kimarekani, wakati zikiuza bidhaa zenye thamani ya dola milioni 584 za kimarekani kwa DRC.

Taarifa hiyo imesema bidhaa zilizouzwa zaidi kutoka EAC kwa DRC ni pamoja na chokaa na saruji, chuma na chuma cha pua, tumbaku, vinywaji, pombe kali na siki, mafuta ya wanyama au mimea n.k.

EABC ni shirika la sekta binafsi la ngazi ya juu zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki likiwa na lengo la kuhimiza mafungamano ya jumuiya ya Afrika mashariki kupitia biashara na uwekezaji.