Msaada wa chanjo za COVID-19 kutoka China wawasili Benin
2022-05-11 09:01:39| CRI

Benin jana ilipokea shehena ya chanjo ya COVID-19 ya Sinovac pamoja na vifaa tiba vilivyotolewa na serikali ya China, ambapo hati ya makabidhiano ilisainiwa na Konsela mkuu wa ubalozi wa China nchini Benin Bw. Yan Yan na mkurugenzi wa wizara ya afya ya Benin Bw. Petas Akogbeto huko Cotonou, Benin.

Msaada huo unajmuuisha dozi za chanjo za Sinovac, sindano, mashine za X-ray, mashine za kufuatilia hali ya mgonjwa, pampu za sirinji za kielektroniki, vitanda vya matibabu, vifaa vya ECG na mashine za kupumulia.

Bw. Yan Yan amesema msaada huo wa China kwa Benin katika sekta ya afya unaonyesha ushirikiano na urafiki wa kina kati ya nchi hizo mbili, haswa katika mapambano dhidi ya janga la COVID-19.