Ethiopia yazindua majaribio ya huduma za mtandao wa 5G
2022-05-11 08:52:16| CRI

Kampuni ya Telecom ya Ethiopia tarehe 9 ilitangaza kuanza majaribio ya huduma za mtandao wa internet wa 5G na kuanza kutoa huduma katika maeneo 6 ya mji mkuu Addis Ababa.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Tamiru katika hafla ya uzinduzi alisema kwamba matumizi ya huduma ya internet ya 5G ni sehemu ya mageuzi ya kidijitali ya Ethiopia. Huduma hiyo inaweza kuboresha uzoefu wa wateja na kusaidia kuinua kiwango cha jumla cha maisha ya Waethiopia kutokana na kasi kubwa ya mtandao, huduma za kuaminika na muda mfupi wa kusubiri.

Kampuni ya Huawei ya China ni mshirika wa kampuni ya Ethiopia Telecom kutoa huduma za 5G na imekuwepo kwenye soko la Ethiopia kwa zaidi ya miaka 20, na itaendelea kushirikiana na kampuni ya Telecom ya Ethiopia kuboresha huduma zao.