Tanzania yapanga kuongeza uvuvi wa dagaa kwenye ziwa Tanganyika
2022-05-11 08:41:46| CRI

Waziri wa mifugo na uvuvi wa Tanzania Bw. Abdallah Ulega, amesema mamlaka ya uvuvi ya Tanzania inapanga kuongeza uvuvi wa dagaa katika ziwa Tanganyika, ili kuongeza thamani ya mnyororo wa thamani kwa vyakula vya baharini.

Akiongea na wavuvi mkoani Kigoma, Bw. Ulega amesema serikali inapanga kuwasaidia wavuvi kupata vifaa vya kisasa vya uvuvi, ikiwa ni pamoja na boti za uvuvi zenye injini na nyavu za kuvulia. Amesema lengo la mpango huo ni kuwawezesha wavuvi kuuza dagaa kwenye soko la ndani na nje kwa bei nzuri na kuboresha maisha yao.

Mwishoni mwa mwaka jana Makamu wa Rais wa Tanzania Bw. Philip Mpango alizitaka nchi zinazochangia ziwa Tanganyika (Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) kushirikiana na kuimarisha hatua za kukabiliana na uharibifu wa mazingira katika ziwa hilo.