Waziri wa mambo ya nje wa Morocco: Afrika imekuwa shabaha kuu ya mashambulizi ya kundi la IS
2022-05-12 09:00:30| CRI

Waziri wa mambo ya nje ya Morocco Bw. Nasser Bourita, amesema Jumatano wiki hii kwenye mkutano wa mawaziri wa muungano wa kimataifa dhidi ya kundi la kigaidi la IS, kuwa Afrika imekuwa shabaha kuu ya mashambulizi ya kundi la IS, ambayo imeshuhudia asilimia 41 ya mashambulizi ya kundi hilo duniani. Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya kigaidi barani humo imeongezeka kwa wastani wa asilimia 40 hadi asilimia 60 ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya janga la COVID-19.

Bw. Bourita amesema vifo vilivyosababishwa na mashambulizi ya ugaidi katika nchi za Afrika kusini mwa Saharan imefikia elfu 30 katika miaka 15 iliyopita, idadi ambayo ni asilimia 48 ya vifo vilivyotokana na ugaidi duniani. Makundi 27 ya kigaidi yaliyowekwa vikwazo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yana makao makuu yake barani Afrika, na eneo la Sahel limekuwa makao ya makundi ya kigaidi yanayokua kwa kasi duniani.

Ameongeza kuwa Afrika imepoteza dola za kimarekani zaidi ya bilioni 171 katika miaka hivi karibuni kutokana na tishio la ugaidi, ambalo sasa limeathiri pwani ya Atlantiki na njia zake za meli.