China, Ethiopia zatarajia kuimarisha ushirikiano kwenye uwekezaji na biashara
2022-05-13 08:38:29| CRI

Ethiopia na China zimefanya mkutano kuhusu ushirikiano wa uwekezaji na biashara unaolenga kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili kwenye nyanja hizo.

Jukwaa la Ushirikiano wa Uwekezaji na Biashara kati ya China na Ethiopia liliandaliwa kwa pamoja na ubalozi wa China nchini Ethiopia, Kamisheni ya Uwekezaji ya Ethiopia (EIC) na Shirika la Kuhimiza Uwekezaji la Wizara ya Biashara ya China huko Addis Ababa.

Kwenye jukwaa hilo, hati ya maelewano (MoU) kuhusu ushirikiano wa uwekezaji kati ya nchi hizo mbili ilisainiwa, ambayo itakuwa utaratibu mpya wa ushirikiano wa kuhimiza uwekezaji na kutoa msukumo mpya kwenye ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.