Tanzania yapanga kuanzisha mahakama zinazotembea ili kupunguza msongamano wa kesi
2022-05-13 08:35:53| CRI

Waziri Mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa jana aliliambia bunge kuwa serikali inapanga kuanzisha mahakama zinazotembea kwenye wilaya zote kwa mwaka wa fedha 2022/23 kwa lengo la kupunguza msongamano wa kesi zinazosubiri hukumu.

Akiongea wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Zuwena Athumani, Bw. Majaliwa amesema mpango huu una lengo la kuharakisha utoaji hukumu, hasa kwenye maeneo ya vijijini. Amesema mahakama ina mpango wa kuongeza idadi ya mahakama zinazotembea kuanzia Julai mosi mwaka huu had Juni 30 mwaka kesho.

Bw Majaliwa amemwagiza waziri wa sheria na mambo ya katiba Bw. Damas Ndumbaro kusimamia uanzishaji wa mahakama hizo wilayani. Amesema mahakama hizo zina ufanisi kwa kuwa zinaweza kufika kwenye maeneo ya mbali ya nchi.