AFC yatoa mkopo wa dola za kimarekani bilioni 2 kusaidia ufufuaji wa uchumi wa Afrika
2022-05-13 08:43:39| CRI

Shirika la Fedha la Afrika (AFC) limetangaza kuzindua mpango wa kutoa mkopo wa dola za kimarekani bilioni 2 kusaidia ufufuaji wa uchumi barani Afrika, wakati wa misukosuko ya kimataifa ikiwa ni pamoja na janga la COVID-19 na mgogoro kati ya Russia na Ukraine.

Shirika hilo limetoa taarifa huko Abuja kuwa mkopo huo utatolewa kwa benki za biashara, benki za maendeleo za kikanda na benki kuu za nchi mbalimbali za Afrika, na kuzipatia fedha taslimu zinazohitajika kugharamia biashara na shughuli nyingine za kiuchumi katika maeneo yao mbalimbali.

Taarifa hiyo imesema benki hizo zitatumia njia iliyothibitishwa na AFC na kupata mikopo kwa viwango vya ushindani.