Balozi mpya wa China nchini Zambia awasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Zambia
2022-05-13 08:36:29| CRI

Balozi mpya wa China nchini Zambia Du Xiaohui amewasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Zambia Hakainde Hichilema mjini Lusaka, na baadaye pande mbili zilifanya mazungumzo marefu.

Balozi Du amesema ni heshima kubwa kwake kupangiwa kufanya kazi Zambia, na kwamba China na Zambia zina urafiki wa kila hali ulioanzishwa na viongozi wa vizazi vilivyopita na kuendelezwa na vizazi vingine, na kujikita mioyoni mwa watu wa nchi hizo mbili.

Amesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, China na Zambia zimefuata kanuni ya kuheshimiana, kunufaishana na kuzingatia maslahi ya upande mwingine.

Rais Hichilema amesema Zambia na China zina urafiki karibu na wenye mafanikio kwenye sekta za uchumi, utamaduni na usalama. Pia ameishukuru China kwa msaada mkubwa iliotoa kwa Zambia kwenye mapambano dhidi ya COVID-19, na kwamba Zambia iko tayari kujifunza kutoka kwa uzoefu wa maendeleo wa China.