Watu milioni 55 barani Afrika waangukia katika umaskini uliokithiri kutokana na janga la COVID-19
2022-05-16 08:43:30| cri


 

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa imesema, janga la COVID-19 limekuwa na athari kubwa barani Afrika ambapo watu milioni 55 waliangukia katika hali ya umaskini uliokithiri mwaka 2020.

Ripoti hiyo ilitolewa katika Mkutano wa mawaziri wa fedha, mpango na maendeleo ya uchumi barani Afrika unaofanyika kuanzia tarehe11 hadi 17 mwezi huu huko Dakar, Senegal. Ripoti hiyo ilichambua sababu ya kuongezeka kwa umaskini na matokeo yake katika kipindi cha mlipuko wa COVID-19.