Bunge la Somalia lamchagua tena rais wa zamani kushika wadhifa huo
2022-05-16 08:33:05| cri

Rais wa zamani wa Somalia Bw. Hassan Sheikh Mohamud amechaguliwa tena kuwa Rais wa kumi wa Somalia, na kumshinda Rais aliyepo madarakani sasa Mohamed Farmajo katika duru ya tatu ya kura iliyofanyika jana katika mji mkuu wa Mogadishu.

Habari zinasema, Bw. Mohamud mwenye umri wa miaka 67, amekuwa rais wa kwanza kuchaguliwa mara mbili katika historia ya Somalia.